Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 03:09

Mazungumzo ya upatanishi kati ya pande hasimu Libya yaonyesha mafaniko


Kaimu Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Stephanie Williams akongea wakati wa ufunguzi wa kongamano la kisiasa huko Gammarth nje ya mji mkuu wa Tunis, uliohudhuriwa na Rais wa Tunisia Kais Saied, Novemba 9, 2020.
Kaimu Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Stephanie Williams akongea wakati wa ufunguzi wa kongamano la kisiasa huko Gammarth nje ya mji mkuu wa Tunis, uliohudhuriwa na Rais wa Tunisia Kais Saied, Novemba 9, 2020.

Viongozi wa pande zilizo hasimiana nchini Libya wamekamilisha duru nyingine mpya ya mazungumzo mjini Tangier Morocco wakati upatanishi ukionyesha kufanikiwa kutanzua mvutano uliolitumbukiza taifa hilo la Afrika Kaskazini katika mapigano ya karibu miaka 10 sasa.

Duru hiyo mpya iliwahusisha maafisa wa baraza kuu la bunge na baraza kuu la taifa.

Mazungumzo hayo ya siku mbili yaliyo malizika Jumanne yaliwahusisha wajumbe 13 wa kila upande wa baraza kuu la bunge la Libya na wawkilishi wa baraza kuu la tafa.

Wajumbe wa baraza kuu la bunge ambalo lilichaguliwa 2014 limegawika kati ya wale wanaounga mkono serikali ya umoja wa kitaifa, GNA, inayotambulika na Umoja wa Mataifa inayoshikilia maeneo ya magharibi ya Libya na wale wanaounga mkono utawala wa mashariki unaoongozwa na kiongozi wa kijeshi aliyeasi Khalifa Haftar.

Ibrahim Abdelaziz Sahad mjumbe wa serikali ya Umoja wa Kitaifa mjini Tripoli anasema wamefikia maridhiano juu ya masuala muhimu.

Sahad anaisema : "Tumefikia maridhiano kamili juu ya masuala mawli tuliojadili, kifungu kuhusiana na misimamo wa kitaifa na uchaguzi wa mamlaka kuu ya utawala. Na suala la pili kuhusu uungaji mkono na msaada wetu kwa majadiliano ya kisiasa yanayo simamiwa na Umoja wa Mataifa ili kuweza kupata mafanikio kamili, na ndio maana tumefanikiwa kabisa juu ya masuala hayo mawili."

Libya imekuwa katika hali ya ghasia na mapigano tangu mwaka 2011 baada ya kupinduliwa kwa kiongozi wa muda mrefu Muammar Ghadafi na waasi walioungwa mkono na ushirika wa NATO.

Bunge la Taifa limegawika ambapo nusu ya wajumbe walikuwa wanakutana mashariki katika mji wa Benghazi na nusu huko magharibi katika mji mkuu wa Tripoli.

Na baada ya mwaka mzima kujaribu kuuchukuwa mji wa Tripoli na kuhusisha mataifa ya kigeni, kiongozi wa kijeshi wa Mashariki Haftar alikubali kutia saini makubaliano ya kusitisha mapigano mwezi Oktoba. Hatua hiyo ndio imefufua juhudi za UN za kutafuta suluhisho la amani kwa mzozo wa Libya.

Khalid Ali Oussad wa serikali ya Umoja wa Kitaifa anasema wamepiga hatua kubwa mbele.

Oussad anasema :"Kamati hii ndogo ya wajumbe 13 kutoka kila upande hivi sasa itachukuwa hatua ya kiutawala na kuanza kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa."

Mazungumzo haya ya wiki hii yanafuatia mazungumzo yaliyo fanyika huko huko Tangier ambapo zaidi ya wabunge 120 waliahidi kukomesha kabisa mgawaniko nchini mwao na kuanza kuitisha vikao vya bunge lililochaguliwa, pindi tu watakaporudi nyumbani.

Mazungumzo ya Tangier yanafuatia mazungumzo yaliyo fanyika mjini Tunis, nchini Tunisia ambako wajumbe walikubaliana kuitisha uchaguzi mkuu Disemba 24 2021, lakini hawajakubaliana bado juu ya nani atakaeongoza kipindi cha mpito kuelekea uchaguzi huo.

XS
SM
MD
LG