Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 19:49

Watu wenye silaha Darfur wavamia ghala la chakula la WFP


Ramani ya Darfur, Sudan
Ramani ya Darfur, Sudan

Maafisa katika mkoa wa Darfur Kaskazini nchini Sudan wametangaza amri ya kutotoka nje usiku baada ya watu wasiojulikana waliokuwa na silaha kuvamia ghala la shirika la chakula duniani, WFP, lililokuwa litumiwa na kikosi cha zamani walinda amani.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatano, Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya tani 1,700 za chakula zilizotarajiwa kulisha watu 730,000 walio katika mazingira hatarishi kwa mwezi mzima zimeibwa kutoka kwenye ghala hiyo katika mji mkuu El Fasher, usiku wa Jumanne.

Wakazi wanaripoti kusikia milio ya risasi karibu na eneo hilo kwa mujibu wa shirika la Habari la serikali la SUNA.

Mtu mmoja kati ya watatu nchini Sudan anahitaji misaada ya kibinadamu.

"Shambulizi kama hilo linadumaza uwezo wa usambazaji wetu kwa watu wenye shida zaidi," alisema hayo mratibu wa maswala ya kibinadamu wa umoja wa mataifa Khardiata Lo Ndiaye.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres pia amelaani shambulizi hilo.

XS
SM
MD
LG