Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 12:44

Wanawake wapitia mateso Darfur


Watu waliokoseshwa makazi Darfur kwenye picha ya awali.
Watu waliokoseshwa makazi Darfur kwenye picha ya awali.

Wanaharakati wa haki za wanawake kutoka magharibi mwa Sudan wanasema kuwa mamia ya wanawake waliokoseshwa makazi kutokana na mapigano huko Darfur wanapitia hali ngumu ya maisha.

Hali hiyo ni kufuatia mapigano ya kikabila kwenye mji wa Al Geneina Darfur magharibi, wakati wakisemekana kupitia hali ya wasi wasi pamoja na msongo wa mawazo kutokana na jukumu kubwa la kulea watoto bila kuwa na waume zao.

Mapigano hayo yaliozuka Aprili yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 200 huku idadi sawa na hiyo iwakiwa wamejeruhiwa. Maelfu ya familia zimepewa hifadhi kwenye mashule, misikiti pamoja na majengo ya serikali.

Waathirika hao wanasemekana kuishi kwenye mazingira magumu kutokana na ukosefu wa huduma za msingi. Kulingana na Umoja wa Mataifa, takriban watu 65,000 wengi wao wanawake na watoto wamekoseshwa makazi kutokana na mapigano hayo.

Sumeya Musa ambaye ni mwanaharakati wa haki za wanawake wakati akizungumza kwenye kipindi cha VOA cha South Sudan in Focus, amesema kuwa wanawake wengi walibakwa au kunyanyaswa kingono wakati wa ghasia hizo ingawa wengi waliamua kunyamaza kwa kuhofia unyanyapaa.

XS
SM
MD
LG