Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 25, 2024 Local time: 12:23

Washutumiwa 13 wa utumiaji silaha wauliwa na polisi Tanzania


IGP SIRRO
IGP SIRRO

Watu 13 wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya kutumia silaha za moto wilayani Kibiti Mkoa wa Pwani inadaiwa wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi.

Polisi wamesema kuwa pia wamekamata bunduki nane, magazini mbili, vitenge na begi katika operesheni hiyo.

Vyanzo vya habari nchini Tanzania vimeripoti kuwa taarifa ya Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro imesema Alhamisi kuwa Agosti 4 katika eneo la Gari Bovu, Kijiji cha Chamiwaleni katika wilaya hiyo polisi walimkamata Abdallah Mbindimbi Abajani akiwa na majeraha maeneo mbalimbali mwilini mwake.

Taarifa hiyo imedai kuwa ilionekana kuwa mshukiwa huyo alikuwa anaendelea kujitibu mwenyewe kwa kificho, na kukubali kuwaonyesha jeshi la polisi sehemu ya mafichoni ambako washukiwa hao wenzake waliopigwa risasi walipokuwa wamejificha ambao alikiri kuwa mshirika wao.

Polisi wamesema katika mapori ya kijiji cha Rungurungu, ulitokea upinzani mkali wa majibizano ya risasi jambo lililosababisha hata Abdallah Mbindimbi Abajani kujeruhiwa kwa risasi sehemu mbalimbali za mwili wake.

Polisi wamesema waliwajeruhi washutumiwa 12 na baadaye walifariki dunia, (akiwemo Abdallah) kwa nyakati tofauti wakati wakipelekwa hospitali. Miili ya watu hao imehifadhiwa kwenye chumba cha maiti hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mauji ya Kibiti yamedumu mwaka wa pili ambapo watu wasiojulikana wamekuwa wakiwashambulia maafisa wa serikali za mitaa, wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na maafisa wa polisi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo afisa wa ngazi ya juu ya upelelezi, watumishi wa idara ya maliasili waliuawakatika wilayani Kibiti mwaka 2017.

Matukio mengine ni kuuawa kwa trafiki polisi wawili katika eneo la Bungu “B” wilayani Kibiti, kumuua diwani wa zamani CCM katika tukio la Kibwibwi wilayani Kibiti na kuua ofisa mtendaji ,mwenyekiti wa mtaa na mkulima katika tukio la Kijiji cha Mangwi wilayani Kibiti.

​
XS
SM
MD
LG