Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 20:21

Watu kadhaa wamejeruhiwa wakiwemo watoto kwa kuchomwa kisu Ufaransa


Eneo ambalo watu walishambuliwa kwa kisu Ufaransa.

Mshambuliaji aliyekuwa na kisu amewachoma watoto kadhaa na mtu mmoja mzima na kusabisha majeraha kwa wengine kabla hajakamatwa.

Shambulizi hilo limetokea katika bustani kando ya mto eneo la mji ulioko kwenye milima ya Alps nchini Ufaransa leo Alhamisi, maafisa wamesema.

Rais wa Ufaransa Emmanul Macron ameeleza shambulizi hilo katika mji wa Annecy kama shambulio la kiuoga kabisa.

Polisi walimkamata mshambuliaji ambaye anaonekana kuwa na umri wa miaka kati ya 30, amesema hayo Waziri wa Mambo ya Ndani Gerald Darmanin.

Polisi imesema watoto wanne walioathiriwa wako chini ya umri wa miaka 5.

Msemaji aliyezungumza na televisheni ya BFMTV amesema mtoto mmoja alishambuliwa akiwa kwenye stroller ya kubeba watoto .

Rais wa bunge la ufaransa , Yael Braun –Pivet alisema: “ kuna baadhi ya watoto wadogo walioko katika hali mbaya na nina wakaribisha nyinyi kuheshimu dakika chache za kukaa kimya kwa ajili yao, kwa ajili ya familia zao, tunatumaini matokeo ya shambulizi hili baya zaidi yasilete huzuni kwa taifa.”

Forum

XS
SM
MD
LG