Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 14:03

Watu 19 wafariki na 26 waokolewa kutokana na ajali ya ndege ya Precision Air, Tanzania


Waokozi wakijaribu kuwatoa abria kwenye ndege iliyopata ajali ya Precision Air
Waokozi wakijaribu kuwatoa abria kwenye ndege iliyopata ajali ya Precision Air

Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa anasema idadi ya walofariki kutokana na ajali ya ndege iliyoanguka kwenye ziwa Victoria imefikia 19.

Alipowasili mjini Bukoba, waziri mkuu Majaliwa, aliwauambia umati wa watu kwamba "Watanzania wote wako pamoja na nyinyi katika kuomboleza vifo vya watu 19 walofariki kwenye ajali hii. "

Ndege hiyo ya Precision Air, ilikuwa inatoka Dar-es-salaam kuelekea Bukoba.

kabla ya hapo wakuu wa mkoa walisema kwamba ndege hiyo ya Precision ATR42 ambayo ina namba za usajili 5HPWF ilikuwa inatoka Dar-es-salaam kuelekea Bukoba ikiwa na jumla ya watu 43.

Katika hao 39 ni abiria, wawili ni wahudumu na 2 ni marubani,” amesema mkuu wa mkoa wa Kagera Albert Chalamila.

wakuu hao walisema watu 26 wameokolewa na kulazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera.

Video kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha watu wakivuta ndege hiyo kwa kutumia Kamba iliyofungwa kwenye ndege huku boti zikiwa zimeizunguka. “Tunachunguza kuona kama tayiri zimeguza chini kwa udongo ili tupate utaalam mwingine wa kuivuta hiyo ndege ili iweze kutoka,” ameeleza Chalamila.

Maafisa wamesema kwamba “kuna mawasiliano kati ya marubani na wasimamizi wa safari za anga.”

XS
SM
MD
LG