Maafisa hawakutoa taarifa ndege hiyo ilikuwa ikitokea wapi au ikienda wapi ajali hiyo ilipotokea ilianguka kiasi cha kilometa 150 kaskazini mwa makao makuu ya jimbo la Mississipi Jackson.
Sababu ya ajali pia bado haijajulikana. Msemaji wa jeshi la majini la Marekani kapteni Sarah Burns amesema ndege hiyo aina ya KC-130 ilipata hitilafu lakini hakueleza zaidi.
Mkurugenzi wa dharura wa kaunty ya Leflore Frank Randle aliwaambia waandishi wa habari kwamba waliopoa miili 16 katika eneo la ajali.