Tillerson alisafiri kutoka Kuwait, ambayo imekuwa ikitafuta suluhisho la mgogoro huo, baada ya kukutana na Emir Sheikh Sabah Al Ahmed Al Sabah.
Mwezi uliopita, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Misri na wengine walikata mahusiano ya kidiplomasia na kuanzisha vikwazo vya ardhini, baharini na angani dhidi ya Qatar, wakiishutumu nchi hiyo kuwa inasaidia ugaidi.
Ratiba ya Tillerson inahusisha kukamilisha kituo chake cha mwisho katika ziara yake huko Saudi Arabia siku Alhamisi
Mshauri wake wa mawasiliano wa ngazi ya juu R. C. Hammond amesema sababu ya ziara yake ni kutafuta njia yoyote itakayo wezesha kutatua mgogoro huu.
Hammond amesema Rais Donald Trump wa Marekani ameweka wazi kuwa lengo lake nambari moja ni kuyafanya mataifa ya kiarabu wachukue hatua zaidi kukomesha ufadhili wa vikundi vya kigaidi.
Baada ya ziara yake ya kwanza nje ya Marekani huko Saudi Arabia, Rais Trump aliishutumu Qatar kwa kusaidia ugaidi katika viwango vya juu. Qatar imekanusha tuhuma hiyo.
Kikundi kinachoongozwa na Saudi Arabia kimeipa Doha masharti 13, ikiwemo wito wa kwamba Qatar ipunguze uhusiano wake na Iran na ifunge kituo cha televisheni cha al-Jazeera kinachofadhiliwa na Qatar.
Qatar imesema iko tayari kufanya mazungumzo lakini kamwe haitokubali kupoteza uhuru wake.