Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 03:37

Watu 13 wafariki baada ya ukuta wa kisima kuanguka India


Waziri Mkuu wa India Narendra Modi
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi

Wanawake na wasichana 13 wamefariki dunia wakati walipokuwa wakiimba na kucheza kwenye sherehe ya harusi, baada ya sehemu ya juu ya ukuta wa kisima kuanguka kutokana na uzito mwingi kaskazini mwa India.

Watu wengine 10 wamejeruhiwa baada ya kuanguka ndani ya kisima hicho, na wamelazwa hospitali katika wilaya ya Utter Pradesh.

Kisima hicho kina urefu wa futi 50 kwenda chini na kilikuwa hakitumiki.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ameandika ujumbe wa tweeter na kutaja tukio hilo kuwa la majonzi makubwa huku akiwaombea afueni waliojeruhiwa.

Uchunguzi unafanyika kuhusiana na tukio hilo, ambalo limetokea karibu kilomita 300 mashariki mwa mji mkuu wa jimbo la Utter Pradesh, wa Luckanow.

XS
SM
MD
LG