Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 18:12

Watatu washinda Tuzo ya Nobel ya Uchumi

Goran K Hansson (K), Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kifalme ya Sweden ya Tafiti za Kisayansi , na wajumbe wa taasisi hiyo Peter Fredriksson (kushoto) and Jakob Svensson, Stockholm, wakitangaza washindi wa tuzo ya Nobel ya Uchumi, Octoba 14, 2019.Karin Wesslen/TT News Agency/via REUTER

Wachumi watatu wameshinda Tuzo ya Nobel ya masuala ya uchumi kutokana na mchango wao wa kupambana na umaskini duniani.

Taasisi ya Sweden ya Tafiti za Kisayansi imetangaza Jumatatu imetoa tuzo hizo kwa Abhijit Banerjee, Mmarekani aliyezaliwa India, Mfaransa – Mmarekani Esther Duflo, na Mmarekani Michael Kremer.

Duflo ni mwanamke wa pili kupata tuzo kwenye fani ya uchumi katika historia.

Taasisi hiyo imesema wachumi hao walianzisha utaratibu mpya wa kuleta njia bora za kupambana na umaskini, wakiangaza masuala madogo kama vile jinsi ya kuboresha afya na elimu ya mtoto.

Washindi hao watagawana tuzo hiyo ya dola 915,300.

XS
SM
MD
LG