Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:13

Wataalam waeleza mafanikio ya chanjo ya polio duniani


Mtoto akipewa chanjo ya polio katika siku ya kuadhimisha kampeni ya kupambana na ugonjwa huo Afghanistan, Septemba 2020.
Mtoto akipewa chanjo ya polio katika siku ya kuadhimisha kampeni ya kupambana na ugonjwa huo Afghanistan, Septemba 2020.

Wakati ambapo idadi ya watu wanaokwepa chanjo inaogezeka, chanjo ya polio imebainika kuwa inafanya kazi. 

Licha ya vikwazo na janga la virusi vya corona, dunia inapata maendeleo katika kutokomeza ugonjwa wa polio.

Kuna wakati mmoja, polio ilisababisha kupooza kwa maelfu ya watoto kila mwaka. Barani Afrika pekee, ugonjwa huo uliwakumba watoto 75,000 kila mwaka. Si hivyo tena hivi sasa.

"Tumefanikisha hatua kubwa sana katika kutokomeza polio ulimenguni huku bara la Afrika likiwa halina virusi vya polio."

Ramani ya Africa
Ramani ya Africa

Chanjo imemaliza polio katika dunia iliyoendelea zaidi ya miaka 50 iliyopita., mwaka 1988, Juhudi za Kutokomeza Polio Ulimwenguni iliamua kufanya hivyo katika nchi zinazoendelea.

Imechukua kazi nyingi sana, watu wa kujtiolea wengi sana, na msaada kutoka kwa wafadhili wengi, lakini hivi sasa, virusi vya polio vipo nchini Afghanistan na Pakistan pekee.

Katika nchi zote hizo mbili, kuna ripoti za kuibuka kwa virusi katika muda wa miaka miwili iliyopita. Nchini Pakistan, watu waliokoseshwa makazi na ghasia na mzozo wamepatiwa makazi katika jamii ambazo zinahuduma dunia za afya na usafi wa mazingira.

Dr. Hamid Syed Jafari mkurugenzi wa kutokomeza polio katika eneo la mashariki mwa Mediterranea kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) anasema, “virusi vya polio havina huruma katika hizi jamii. Unafahamu kuwa viko katika eneo hili ambalo lina watu wengi sana, unajua, huduma duni za usafi wa mazingira na afya. Hali hii inabainisha ni nzuri kwa virusi vya polisi kuzaliana na kushamiri, kwa kweli vimekaa huko.”

Jafari anasema program ya kutokomeza virusi hivi saa imezisaidia hizi jamii kukidhi mahitaji mengi zaidi ya afya.

Nchini Afghanistan, Taliban hairuhusu utoaji wachanjo kwa watu wengi au wa nyumba kwa nyumba.

Carol Pandak wa Rotary Intternational Polio Plus Program anasema, “kama hufanyi kampeni ya nyumba kwa nyumba, pengine unawezaje kufanya kampeni ya chanjo na kwenye vituo vidogo vidogo? Pengine vituo vidogo vya chanjo hasa katika jamii ili familia hazina haja ya kusafiri ya kwenda umbali mrefu ili watoto wao wapatiwe chanjo. Tunajaribu kuwa wabunifu na kuangalia njia za kusukuma mbele juhudi zetu za kutokomeza majanga mawili yaliyobaki katika nchi.”

Kwa sababu ya janga la virusi vya corona, watoa chanjo katika nchi nyingi inawalazimu kuvaa barakoa na glovu.

JuhudI za kutokomeza polio ulimwenguni zinakaribia , na mafanikio ya kihistoria ni makubwa, lakini mpaka ugonjwa utakapotokomezwa kabisa nchini Afghanistan na Pakistan, kwa mara nyingine tena unaweza kusambaa ulimwenguni.

COVID-19 inatoa mfano mzuri kabisa jinsi ya ambavyo virusi vinavyoweza kusambaa.

XS
SM
MD
LG