Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 09:33

Wastaafu 120 wa Jeshi Wasisitiza Umuhimu wa Diplomasia


Zaidi ya wastaafu 120 wa jeshi la Marekani, kati yao wakiwemo majenerali na maadmirali, wanasisitiza Bunge lisipunguze matumizi katika nyanja za diplomasia na misaada ya nje.

Wameeleza wasiwasi wao kwamba huenda vitengo hivyo viwili vya serikali vikawa vimelengwa na pendekezo la mara ya kwanza la bajeti ya Rais Donald Trump.

Atakapokuwa anazindua bajeti ya Jumanne mbele ya Bunge, Trump anategemewa kuomba dola bilioni 54 ambazo zitatumika kuboresha jeshi na hivyo kupunguza bajeti ya matumizi ya kawaida kufidia ongezeko hilo. Wachambuzi wa bajeti wanasema punguzo hilo linaweza hasa kulenga wizara ya mambo ya nje na idara ya kulinda Mazingira.

Katika barua Jumatatu kwa viongozi wa Warepublikan na Wademokrat, maafisa wastaafu wameandika kwamba “ Kuendeleza na kuimarisha diplomasia na maendeleo sambamba na ulinzi wa taifa ni muhimu katika kuifanya Marekani iendelee kuwa salama.”

Viongozi hao wa zamani wa jeshi wameandika kwamba uzoefu umewafundisha kwamba matatizo mengi ya nchi hayawezi kutatuliwa tu kwa kutumia nguvu za kijeshi.

Wizara ya Mambo ya Nje, shirika la USAID, Shirika la Millennium Challenge Corporation, Shirika la Peace Corps na mashirika mengine ya maendeleo ni muhimu katika kuzuia migogoro na kupunguza hatari ya kuwaweka wanajeshi wetu hatarini.

Baadhi ya viongozi wastaafu wa jeshi la Marekani maarufu wamesaini barua hiyo, akiwemo Jenerali David Petraeus, kiongozi wa vikosi Afghanistan na Iraq na Admirali wa jeshi la majini James Stavridis, ambaye pia aliwahi kuwa mkuu wa majeshi ya Ushirika ya NATO.

Bajeti ya jeshi la Marekani ni takriban dola bilioni 600. Marekani inatumia kiasi cha dola bilioni 54 kila mwaka katika juhudi za misaada ya kimataifa.

Bunge halitotakiwa kukubali pendekezo la bajeti ya Trump na anatarajiwa kuwa na mahojiano kadhaa na Bunge kuielezea bajeti yake.

Barua hiyo iliratibiwa na kuchapishwa Jumatatu kwenye mtandao na Shirikisho la Uongozi la Kimataifa, ni kikundi kinachosimamia diplomasia na msaada wa nje.

XS
SM
MD
LG