Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 05:53

Hotuba ya Trump Kuibua Masuala ya Msingi, Ndani na Nje ya Nchi


Rais Donald Trump cadena Fox
Rais Donald Trump cadena Fox

Maafisa wa White House wameahidi kuwa hotuba ya Rais Donald Trump ya kwanza kwa Bunge la Marekani Jumanne jioni “itajikita katika kutatua matatizo halisi ya watu.”

“Rais atawajulisha kwamba msaada uko njiani,” afisa wa juu wa uongozi huo amewaambia waandishi wa habari wakiwa White House Jumatatu jioni.

Hotuba ya Trump ataitoa Jumanne jioni (9pm EST) kwa mabaraza yote ya Bunge, ina anwani “kuimarishwa tena kwa Marekani” na kimsingi itakuwa inahusu nafasi za kiuchumi na kuwalinda watu wa Marekani,” amesema afisa wa juu.

Kutakuwa na mambo yanayohusu sera ya nje katika hotuba hiyo, maafisa wa uongozi huo wamesema lakini hawategemei nchi kadhaa kutajwa.

Lakini Trump, kwa mujibu wa maafisa hao, atatoa sababu za kujitoa kutoka katika nchi 12 za umoja wa kibiashara wa Trans-Pacific Partnership, ikiwa ni sehemu ya makubaliano madhubuti ya kibiashara ambayo hayajawahi kupitishwa na Bunge' yaliyochukua miaka mingi kufanya mazungumzo na kwa sehemu kubwa yalikuwa yanaongozwa na Washington na Tokyo.

Uhamiaji ni moja ya maeneo Mugumu

Kwa jumla hotuba hiyo “itatoa dira ya matumaini kwa taifa,” msemaji wa White House Sean Spicer amesema mapema katika mkutano wake na waandishi unaofanyika kila siku.

Spicer ameongeza kuwa alikuwa anamatumaini kwamba rais atapata “ mapokezi mazuri na yenye kutia nguvu” kutoka kwa wawakilishi wa Bunge, wakiwemo Wademokrat.

Maoni ya Wademokrati

Kiongozi wa wachache katika Baraza la Seneti Chuck Schumer na kiongozi wa wachache katika Bunge, Nancy Pelosi, wakiwa katika klab ya waandishi Marekani, walijaribu kukosoa hotuba ya rais mapema.

“Donald Trump anataka kuwafanya watu waamini wahamiaji wote ni magaidi na wahalifu,” Schumer amesema.

Msimamo wa Trump ni kubadilika kabisa kwa msimamo wa vyama vyote viwili; Republikan na Demokratkwa miongo mingi juu ya suala la kuheshimu wahamiaji,” ameongeza Pelosi.

Punguzo la kodi, budget

Wabunge wa Republikan wanasema wanategemea kusikia hasa marekebisho ya kodi na afya, ikiwa ni maelezo kuhusu nyongeza ya asilimia 10 kwa ajili ya matumizi ya ulinzi—itayogharimu dola bilioni 54—na kupunguza budget katika maeneo mengine kwa kiwango hicho.

Rais na Warepublikani katika bunge “ kwa pamoja wanakubaliana kufuta Obamacare na kupunguza kodi na usalama wa mpakani na kuboresha kanuni zilizokuwepo, kwa hivyo hayo ndio mambo atayoelezea ilikuweza kuwaleta Warepublikan pamoja,” mchambuzi John Fortier wa Kituo cha Ushirikiano wa vyama katika Sera (BPC).

Msaada wa Marekani nchi za nje unategemewa kulengwa hasa na hotuba hiyo. Kitendo cha kupunguza msaada huo kinapingwa na maadmirali wastaafu 121 na majenerali, ambao wamesema katika tamko lao Jumatatu “ kuipa nguvu na kuinyanyua diplomasia na maendeleo, sambamba na ulinzi, ni muhimu katika kuifanya Marekani iwe salama.

Msaada wa Marekani kwa nchi nyingine ni asilimia 1 ya bajeti yake, ikimaanisha itabidi baadhi ya maeneo ya bajeti yapunguzwe kwa kiwango kikubwa kufidia hilo.

XS
SM
MD
LG