Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 10, 2024 Local time: 11:36

Wapalestina 6 wauawa katika shambulizi la Israel kaskazini mwa Gaza

Eneo la shambulizi lililofanyika Jumamosi tarehe 29 Juni, 2024 katika kitongoji cha al-Mawasi mjini Rafah, kusini mwa Gaza (Picha na Eyad BABA / AFP)
Eneo la shambulizi lililofanyika Jumamosi tarehe 29 Juni, 2024 katika kitongoji cha al-Mawasi mjini Rafah, kusini mwa Gaza (Picha na Eyad BABA / AFP)

Vikosi vya Israel Jumapili vimesonga kwenye kitongoji cha Shejaia kaskazini mwa Gaza huku pia vikipenya magharibi na kati mwa Rafah, upande wa kusini, na kuua takriban wapalestina 6, pamoja na kuharibu majengo kadhaa, mkazi mmoja amesema.

Vifaru vya Israel vilivyorejea Shejaia siku nne zilizopita vilirusha makombora kwenye majengo kadhaa, huku wakazi wakiachwa wamekwama ndani , ripoti zimeongeza.

Jeshi la Israel limesema kuwa vikosi vyake vimeua wapalestina kadhaa, kupata silaha pamoja na kuharibu miundomsingi ya kijeshi ya Wapalestina kwenye eneo hilo.

Jumamosi jeshi hilo limetangaza vifo vya wanajeshi wake wawili kaskazini mwa Gaza.

Kitengo chenye silaha cha Hamas pamoja na kundi la wanamgambo la Islamic Jihad, wameripoti mapigano makali kwenye miji ya Shejaia na Rafah.

Forum

XS
SM
MD
LG