Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 12, 2024 Local time: 03:08

Jeshi la Israel limefanya mashambulizi ya anga kaskazini mwa Gaza


Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu

Jeshi la Israel leo ijumaa limesema lilifanya mashambulizi yaliyosaidiwa na mashambulizi ya anga huko kaskazini mwa Gaza, na kuua darzeni wa wanamgambo katika eneo ambalo ilitangaza kuharibu muundo wa uongozi wa Hamas miezi kadhaa iliyopita.

Operesheni hiyo huko Shujaiya, pembezoni mwa Gaza City, limesababisha vifo vingi, mashahidi na madaktari walisema Alhamisi wakati operesheni ilipoanza. Mapigano mapya upande wa kaskazini mwa Gaza yanafuatia matamshi ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ya Jumapili ambapo alisema kuwa awamu ya vita vikali inapungua baada ya karibu miezi tisa.

Wataalamu wanasema wanatabiri kuwa kuna uwezekano wa muda mrefu wa awamu ijayo. Omer Dostri, mtaalamu wa kijeshi katika Taasisi ya Mkakati na Usalama ya Jerusalem, alisema anatarajia jeshi kupunguza uwepo wake wa ardhini, na kuongeza matumizi ya ndege zisizo na rubani na ndege za kivita ili kuliangamiza zaidi kundi la Hamas.

Leo Ijumaa katika eneo la Shujaiya mwandishi wa shirika la habari la AFP alishuhudia shambulio la anga na kushuhudia moshi ukiongezeka. Ufyatuaji makombora ulisikika.

Forum

XS
SM
MD
LG