Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 10:59

Waokoaji Himalaya wapata miili zaidi wakati vifo vikifikia 50


Watu wakipita eneo la bwawa lililoharibiwa na kuanguka kwa theluji huko kijiji cha Raini Chak Lata , wilaya ya Chamoli, kaskazini mwa jimbo la Uttarakhand India, 7 Februari 2021. (Foto: Reuters)

Waokoaji wamepata miili mingine zaidi tisa katika eneo la mafuriko ya ghafla katika mkoa wa kaskazini ya India kwenye milima ya Himalaya, wiki moja baada ya janga hilo kutokea, na hivyo idadi ya vifo kufikia 50 wakati zaidi ya watu 150 bado hawajulikani waliko, maafisa wamesema.

Mafuriko ya ghafla katika jimbo la Uttarakhand, yalitokea na kile wana sayansi wamesema huwenda ikawa imesababishwa na kuporomoka kwa kipande kikubwa cha thaluji kilicho kutoka mlimani, na kusababisha maji, mawe na vifusi kumiminika na kuja chini katika bonde la mto Dhauliganga, na kimeharibu mabwawa na madaraja.

Waokoaji wanatumia mashine nzito za kuchimbia kuharakisha kuwatoa darzeni ya wafanyakazi wa ujenzi waliokwama katika handaki linaloungana na mradi wa umeme wa maji unaojengwa na shirika la serikali la National Thermal Power Corporation.

“Bado hatujakata tamaa kabisa. Tuna matumaini ya kupata manusura zaidi,” afisa mwandamizi wa serikali katika mkoa, Swati Bhadoriya ameliambia shirika la habari la Uingereza Rueters. Maafisa wa serikali wanasema watu 154 hawajulikani waliko.

Mandhari ya milima ya Himalaya
Mandhari ya milima ya Himalaya

Wataalam wameonya kuwa kunauwezekano bado wa kiwango kikubwa cha majabali, vifusi, barafu na maji yakaporomoka kutoka milimani, na kufanya juhudi za zoezi la uokoaji kuwa hatari zaidi.

Uttarakhand siku zote inakabiliwa na mafuriko ya ghafla na maporomoko ya theluji. Janga hili limeibua wito kutoka kwa vikundi vya mazingira kutizama upya miradi ya umeme katika eneo lenye mazingira hatari ya milima.

Timu ya wana sayansi wanachunguza iwapo kipande cha theluji cha mlima wa Himalaya kilianguka ndani ya maji na kusababisha mafuriko.

Milima ya Himalaya ya India ina theluji takriban 10,000. Uttarakhand yenyewe ina theluji hadi 1,495 na nyingi zinayayuka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa kuwa na joto zaidi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG