Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 22, 2025 Local time: 00:28

Dunia yasherehekea siku ya wapendanao, Valentine


Wapenzi na afisa wa serikali ya mtaa, wakiwa wamepanda tembo, aliyesimamia wakipokea leseni zao za ndoa. jimbo la Chonburi, Thailand, Feb. 14, 2021.
Wapenzi na afisa wa serikali ya mtaa, wakiwa wamepanda tembo, aliyesimamia wakipokea leseni zao za ndoa. jimbo la Chonburi, Thailand, Feb. 14, 2021.

Dunia nzima hii leo inaadhimisha siku ya wapendanao wakibadilishana ujumbe, mawaridi na chokleti kueleza upendo wao. 

Miongoni mwa sherehe hizo huko Thailand wapenzi 59 nchini Thailand walifungishwa ndoa wakiwa wamepanda tembo Jumapili, katika sherehe za Siku ya Valentine ya kila mwaka kwenye bustani ya maua katika jimbo moja mashariki ya Bangkok.

Shirika la Habari la Reuters linaripoti kwamba wacheza ngoma na bendi ya muziki iliongoza msafara wa tembo na wapenzi hao na afisa wa serikali ya mtaa, akiwa amepanda tembo, aliyesimamia kusaini leseni hizo za ndoa.

“Kwa upande wangu nimekuwa nikipanga kwa muda mrefu iwapo nitatakiwa kusaini leseni ya ndoa siku moja, ni lazima iwe ni katika tukio la namna ya kipekee,” amesema Patiphat Panthanon, miaka 26, akiwa pembeni ya biharusi wake.

Ndoa zinazo fanyika juu ya tembo ni tukio la kila mwaka katika bustani ya Nong Nooch Tropical katika jimbo la Chonburi na kawaida huvutia hadi wapenzi 100 wanaotaka kuoana. Lakini mwaka huu kwa sababu ya janga la Corona, idadi imekuwa ndogo.

Kampon Tansacha, rais wa Bustani ya Nong Nooch Tropical, amesema kuwa kutokana na utaratibu wa masharti makali ya kuwakagua wageni, watu walikuwa wanahisi ni salama zaidi na wameanza kuja kutembelea uwanja wa bustani ya maua, ambapo huonyesha aina mbalimbali za ubunifu wa mabustani kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

XS
SM
MD
LG