Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 22:36

Changamoto Mbali Mbali Zachangia kwa Wanawake Kutowania Uongozi Kenya


Wanawake kutoka Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi wakishiriki maandamano ya mwanamke Nairobi, Kenya Oktoba 13, 2015.
Wanawake kutoka Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi wakishiriki maandamano ya mwanamke Nairobi, Kenya Oktoba 13, 2015.

Ushiriki wa wanawake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2013 nchini Kenya ulikuwa wa chini licha ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2010.

Takwimu zinaonyesha kuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2013 jumla ya wanawake 19 tu kati ya wagombea 237 wa nyadhifa za ugavana na useneta ndiyo walipigania nafasi hizo na hakuna aliyechaguliwa.

Vile vile kati ya wabunge 290 wa bunge la taifa ni asilimia 5.5 na kwa nafasi 1450 za wadi ni wanawake 88 ambao ni sawa na asilimia 6 waliochaguliwa kama wanawake.

Uwakilishi wa kisiasa wa wanawake nchini Kenya ni asilimia 15, ikilinganishwa na mataifa ya Afrika ikiwa Rwanda ni asilimia 56, Afrika Kusini ni asilimia 42, Tanzania ni asilimia 36 na Uganda ni asilimia 35.

Japo asilimia 15 ya Kenya ni afueni ikilinganishwa na asilimia 9.8 katika bunge la kumi.

Aidha uoga na kutojiamini miongoni mwa wanawake Kenya ni changamoto kwa wao kunyakua nyadhifa za kisiasa.

Mbali na sheria ya kikatiba kutoa fursa kwa wanawake kushiriki nafasi za kisiasa, idadi kubwa ya wanaopiga kura nchini Kenya ni wanawake.

Naibu gavana wa kaunti ya Kwale, pwani ya Kenya, Fatuma Achani ataja uoga na tamaduni za mwanamke kuonekana dhaifu kumechangia idadi ndogo ya wanawake.

please wait

No media source currently available

0:00 0:06:05 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kati ya kaunti 47 nchini Kenya ni kaunti 9 tu zilizo na manaibu magavana wanawake, tatu zikitoka pwani ya Kenya.

Bi Achani aelezea jinsi kaunti zilizo na manaibu magavana zinavyofanya kazi kama njia ya kuvutia wananchi kuunga mkono wanawake wanaosimama kupigania nyadhifa za kisiasa.

XS
SM
MD
LG