Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:41

Wanawake sita wateuliwa katika Baraza la Mawaziri Kenya


Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amekamilisha Ijumaa uteuzi wa baraza la mawaziri na wanasubiri kuidhinishwa na bunge la nchi hiyo.

Katika uteuzi huo kuna jumla ya wanawake sita waliopewa nyadhifa mbali mbali katika baraza hilo.

Monica Juma ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Amina Mohammed ameteuliwa Waziri wa Elimu, Margaret Kobia ameteuliwa kuwa Waziri wa Vijana na Utumishi wa Umma, Racheal Omamo ameteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi, Sicily Kariuki ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya na Farida Karoney ameteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi ambaye ni mwanahabari mkongwe.

Hatua hii ni kufuatia ushindi wake Kenyatta katika uchaguzi wa urais 2017.

Mawaziri wa zamani walioteuliwa kuwa mabalozi ni Judi Wakhungu - Ufaransa, Cleopa Mailu - Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Dan Kazungu - Tanzania, Phylis Kandie - Ubelgiji, Luxemburg na Umoja wa Ulaya na Willy Bett - India

Wengine Jacob Kaimenyi -UNESCO, Paris, na Hassan Wario - Austria.

Orodha kamili ya mawaziri :

Adan Mohammed - Viwanda

Amina Mohammed - Elimu

Charles Keter - Kawi

Eugene Wamalwa - Ugatuzi

Farida Karoney - Ardhi

Fred Matiangi - Masuala ya Ndani na Usalama

Henry Rotich - Fedha (Hazina Kuu)

James Macharia - Uchukuzi

John Munyes - Madini na Mafuta

Joseph Mucheru - Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

Keriako Tobiko - Mazingira

Margaret Kobia - Vijana na Utumishi wa Umma

Monica Juma -Mambo ya Nje

Mwangi Kiunjuri - Kilimo

Najib Balala - Utalii

Peter Munya - Jumuiya ya Afrika Mashariki

Racheal Omamo - Ulinzi

Raphel Tuju - Waziri (Bila wizara kwa sasa)

Rashid Achesa - Michezo

Sicily Kariuki - Afya

Simon Chergui - Maji

Ukur Yattany - Leba

XS
SM
MD
LG