Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Machi 19, 2025 Local time: 19:23

Wanamgambo washambulia magari kwa risasi na kuua watu nchini Cameroon


Wanajeshi wa Cameroon
Wanajeshi wa Cameroon

Wanamgambo wenye silaha walisimamisha, na kuyachoma magari, na kuwafyatulia risasi abiria, wakati wa shambulio dhidi ya kijiji kimoja katika eneo Linalozungumza Kiingereza, la Kusini Magharibi mwa Cameroon siku ya Alhamisi, wakaazi na ripota wa shirika la habari la Reuters walisema.

Watu wanaotaka kujitenga katika sehemu zinazozungumza Kiingereza nchini Cameroon, wamekuwa wakipigania kuanzishwa kwa taifa huru liitwalo Ambazonia, tangu mwaka 2017.

Wamekuwa wakifanya mashambulizi, utekaji nyara na mauaji katika maeneo ya Kaskazini Magharibi na Kusini Magharibi.

Wakazi walioonekana kuwa na wasiwasi walikusanyika na kuzunguka mabaki, yaliyojaa matundu ya risasi, ya gari lililoungua katika kijiji cha Muea, eneo la Kusini Magharibi, siku ya Alhamisi, wakati wanaume wawili wakiutoa mwili uliokuwa umefungwa na blanketi.

Ndugu na jamaa waliokuwa wakilia walitambua na kuchukua miili miwili, kwa mujibu wa ripota wa Reuters katika eneo la tukio.

Wakazi walisema washambuliaji walifika mapema asubuhi, katika wiki ambayo shule zilifunguliwa baada ya mapumziko ya majira ya joto, na kwamba watu kadhaa waliuawa.

Forum

XS
SM
MD
LG