Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 20:10

Mafisa wa serikali ya Cameroon waliyotoweka wapatikana kwenye kaburi la halaiki


Timu ya kundi la kijeshi la Cameroon linalopambana na uingizaji haramu wa bunduki nchini likiwa mjini Garoua. Picha ya maktaba.

Maafisa wa jeshi wa Cameroon wamesema Jumanne kwamba wamepata kaburi la halaiki karibu na mpaka wa Nigeria, likiwa na miili ya raia 9 wakiwemo maafisa 5 wa serikali ambao walitekwa nyara na waasi mwezi Juni 2021.

Maafisa wa serikali walielekezwa kwenye kaburi hilo na mpiganaji wa uasi aliyeshiriki mauaji hayo lakini akajisalimisha na kujiunga na kituo cha upokonyaji silaha na urekebishaji tabia.

Jeshi la Cameroon limesema kwamba maafisa wa serikali wamefukua miili kutoka kwa kaburi hilo lililopo umbali wa takriban kilomita 20 kutoka mji wa Ekondo Titi ambao unapatikana kwenye eneo la kiutawala la Ndian karibu na mpaka wa Nigeria.

Ripoti zimeongeza kwamba miili Iliyopatikana ilisafirishwa kwa kutumia magunia kutoka kwenye msitu. Kwa muda sasa waasi wamekuwa wakidai kuhusika katika utekaji nyara wa maafisa hao, kwa madai kwamba walikuwa wanashirikiana na serikali kuu yenye makao yake makuu mjini Yaounde.

Mozozo wa Cameroon ulianza 2017 baada ya walimu na mawakili kutoka maeneo ya Kaskazini magharibi na Kusini magharibi ambako lugha ya kiingereza inatumika, kuanza kudai kuwa walikuwa wametengwa na wale wanaotumia kifaransa na ambao ni wengi.

Jeshi lilijibu kwa kuanzisha msako, wakati waasi wakichukua silaha na kudai kulinda raia wao wanaozungumza kiingereza.

Ghasia hizo zimeua takriban watu 6,000 na kusababisha wengine zaidi ya laki 7 kutoroka makwao kulingana na shirika la kutoa misaada la International Crisis Group.

Forum

XS
SM
MD
LG