Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 09:57

Wanajihadi wauwa na kuteketeza kijiji Msumbiji


Wakaazi wa jimbo la Cabo Delgado wakishusha mizigo wakati walipokuwa wakirejea katika eneo hilo Septemba 30. 2022 .Camille LAFFONT / AFP
Wakaazi wa jimbo la Cabo Delgado wakishusha mizigo wakati walipokuwa wakirejea katika eneo hilo Septemba 30. 2022 .Camille LAFFONT / AFP

Shambulizi la wanajihadi katika kijiji cha Ntontwe kaskazini mwa Msumbiji limesababisha vifo vya watu watatu na kuchoma moto darzeni ya nyumba na biashara, vyanzo vya usalama na maafisa wa eneo hilo wamesema Ijumaa.

Kijiji hicho kilichopo katika barabara kuu inayoliunganisha eneo la kaskazini kashariki na kusini mwa jimbo tete la Cabo Delgado —limekuwa likishambuliwa mara kadhaa na wanajihadi.

“Kijiji chetu kimeshambuliwa. Nyumba yangu imetetekea kwa moto, Jumla ya nyumba 43 katika kijiji chetu zimeteketezwa kwa moto na watu watatu wameuawa,” amesema kiongozi wa kijiji cha Ntontwe, alipokuwa akilielezea shambulio hilo.

Vyanzo vya usalama vimethibitisha idadi hiyo ya vifo.

Kijiji hicho kipo takriban kilometa 20 Kusini mwa Chinda, eneo ambalo kuna kambi kubwa ya jeshi la Rwanda, waliopelekwa kupambana na mashambulizi ya makundi yenye silaha, ambayo yamekuwa yakilisumbua jimbo hilo tangu Oktoba 2017.

Lakini walichelewa kuwasili kuzuia shambulio la Ntontwe.

“Wanajeshi wa Rwanda walikuja kutusaidia, lakini walipowasili wanamgambo walikuwa tayari wameshafanya yote waliyokuwa wanataka kuyafanya,” kiongozi wa kijiji alisema.

Kijiji cha Ntontwe kimetelekezwa kwa miaka mingi, lakini mwaka jana wakaazi wameanza kurejea, wakati mwezi Oktoba mamlaka ya eneo hilo imewaweka watu takribani 5,000.

Forum

XS
SM
MD
LG