Ujumbe wa MINUSMA ambao umekuwepo kwa muongo mmoja, awali ulitakiwa ukabidhi kambi zake za Gao na Timbuktu kwa mamlaka ya Mali mwezi Januari. Lakini hali mbaya ya kiusalama katika eneo hilo linalokabiliwa na mashambulizi wanajihadi yaliyosababisha kuondoka haraka Timbuktu.
“Kutokana na ukosefu wa suluhu ya usalama wa ndani ya kambi ya MINUSMA iliyoko Timbuktu, imetulazimu tufunge kambi hii haraka” chanzo cha Umoja wa Mataifa ambacho kiliomba kisitajwe jina kiliiambia AFP.
Gavana wa mkoa Bakoun Kante alionekana akiushukuru Umoja wa Mataifa wakati wa hafla rasmi ya makabidhiano siku ya Alhamis, iliyotangazwa na kituo cha televisheni cha ORTM
Utawala wa kijeshi wa Mali uliitaka MINUSMA iondoke haraka mwezi Juni mwaka jana kutokana na kuzorota kwa mahusiano.
MINUSMA imepoteza wanajeshi 180 katika kipindi cha miaka kumi, ilikuwa ikijaribu kulinda amani katika taifa hilo la Sahel lenye matatizo makubwa ya ghasia za wanajihadi.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP
Forum