Hatua hii imefuata baada ya Kinshasa kukataa kuongeza muda wa mkataba.
Mataifa saba ya EAC yaliyapeleka majeshi Novemba mwaka 2022, katika eneo ambalo limeelemewa na ghasia, kwa mwaliko wa mamlaka ya DRC, kuyakomboa maeneo yaliyokuwa yamechukuliwa na waasi wa kundi la M23.
Lakini mustakbali wa upekaji majeshi ulitiliwa mashaka, baada ya Rais Felix Tshisekedi na wakazi wa eneo hilo kuyashutumu majeshi hayo kufanya kazi na waasi badala ya kuwalazimisha kuweka chini silaha.
Waandisi wa habari wa AFP mapema siku ya Ijumaa waliliona kundi la wanajeshi wa Sudan Kusini likiondoka katika mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, Goma.
Wanajeshi waliondoka kutoka uwanjwa wa ndege wa Goma saa kumi na moja asubuhi kuelekea Juba.
Wanajeshi wa Uganda na Burundi pia wanapaswa kuondoka katika kipindi cha wiki zijazo, chanzo hicho kilisema, huku majeshi hayo ya kikanda yanatarajiwa kukamilisha kuondoka kwao ifikapo Januari 7.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP
Forum