Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 04:47

Wanajeshi wa Kenya waanza kuondoka Goma, kabla ya muda wa kikosi cha EACRF kumalizika


Wanajeshi wa Kenya kutoka kikosi cha EACRF waonekana wakiondoka kutoka uwanja wa ndege wa Goma, Kivu Kaskazini.
Wanajeshi wa Kenya kutoka kikosi cha EACRF waonekana wakiondoka kutoka uwanja wa ndege wa Goma, Kivu Kaskazini.

Mamia ya wanajeshi wa Kenya wameondoka kutoka mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jumapili mchana, ikiwa ishara ya kuanza kuondoka kwa kikosi cha Jumuia ya Afrika Mashariki, baada ya Kinshasa kukata kuongeza muda wake ili kupambana na kundi la M23.

Rais Felix Tshisekedi wa Kongo mara kwa mara amekua akikosoa kikosi hicho cha dharura cha kikanda, EACRF, tangu kupelekwa huko Novemba 2022, kwa kushindwa kutekeleza makubaliano ya kukimaliza kundi la waasi la M23, kinachodai kutetea maslahi ya watutsi.

Ikulu ya Kinshasa ilitangaza mwisho wa mwezi wa Novemba, kwamba haitongeza tena muda wa kikosi hicho ambao unamalizika Disemba 8.

Msemaji wa EACRF amethibitisha kwamba wanajeshi wanarudi Nairobi wakipanda ndege mbili kutoka Goma lakini hakutoa maelezo zaidi ikiwa wanajeshi wengine wa kikosi hicho kutoka wa Uganda, Burundi na Sudan Kusini wataondoka karibuni.

Wanajeshi wa Kenya waloshiriki kwenye kikosi cha kikanda EACRF wakiondoka kutoka uwanja wa ndege wa Goma, mashariki ya DRC
Wanajeshi wa Kenya waloshiriki kwenye kikosi cha kikanda EACRF wakiondoka kutoka uwanja wa ndege wa Goma, mashariki ya DRC

Kikosi kipya kutoka Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC kinatazamiwa kuchukua nafasi ya kikosi cha Afrika Mashariki, lakini tarehe ya kuwasili kwa wanajeshi hao na muda wa kubaki hukio haujatangazwa bado.

Mabadiliko hayo ya usalama yanamulika jinisi hali ni ngumu kuleta utulivu katika majimbo ya mashariki ya Kongo ya Kivu Kaskazini na Ituri, ambako serikali imetangaza hali ya dharura kwa miaka miwili sasa ili kuweza kukabiliana na kuongezeka kwa ghasia za wanamgabo.

Kulingana na Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM, ghasia katika majimbo hayo yamesababisha karibu watu milioni 6 laki 9 kupoteza makazi yao na kubaki ndani ya nchi.

Ripoti hii imetayarishwa kutokana na habari za Reuters na AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG