Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 10:05

Wanajeshi wa AMISOM watibiwa Mombasa


Walinda amani wa Umoja wa Afrika Somalia AMISOM wakilinda jengo moja la serikali mjini Mogadishu.
Walinda amani wa Umoja wa Afrika Somalia AMISOM wakilinda jengo moja la serikali mjini Mogadishu.

Wanajeshi 14 waliojeruhiwa katika mapigano mjini Mogadishu siku ya Jumatano wamefikishwa Mombasa kwa matibabu

Maafisa wa jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika huko Somalia, AMISOM, walizusha hali ya taharuki siku ya Ijumaa huko Mombasa, baada ya kufahamika kwamba wanajeshi wake wanatibiwa mjini humo .

Vyombo vya habari vya Kenya vilitangaza habari hizo, baada ya kupata picha zilizowaonyesha wanajeshi hao 14, waliojeruhiwa wakati wa mapigano makali siku ya Jumatano huko Mogadishu, wakiwasili mjini Mombasa.

Wasi wasi ulizuka kutokana na hofu kwamba, huenda hospitali wanapotibiwa wanajeshi hao ikavamiwa na wanaharakati wa Kisomali.

Hali kama hiyo ilitokea huko mjini Mandera Kaskazini Mashariki mwa Kenya, pale wanaharakati walipopata habari kwamba, kuna baadhi ya wanajeshi wa AMISOM wanatibiwa katika hospitali moja mjini humo.

Mwandishi habari wa kituo cha Baraka FM mjini Mombasa anasema, usalama wa wanajeshi hao ni muhimu hasa kwa vile kuna wakimbizi wengi wa kisomali mjini Mombasa.

XS
SM
MD
LG