Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 11:30

Serikali ya Somalia yakomboa Beti Hawo


Mwanajeshi wa Umoja wa Afrika Mogadishu
Mwanajeshi wa Umoja wa Afrika Mogadishu

Majeshi ya serikali na wanamgambo watimua al-Shabab Beti Hawo

Maafisa wa Somalia wanasema majeshi ya serikali yamekomboa mji wa Belet Hawo kutoka kwa wanamgambo wa al-Shabab baada ya mapigano yaliyochukua saa kadhaa.

Maafisa hao wamesema Jumamosi kuwa vikosi vya ulinzi na wanamgambo wanaounga mkono serikali ya mpito waliweza kuudhibiti tena mji huo ulioko karibu na mpaka wa Kenya.

Afisa wa kijeshi, aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa wanamgambo 20 wa al-Shabab waliuawa katika mapigano hayo.

Kudhibitiwa tena na serikali kwa mji wa Belet Hawo ni hatua moja ya kampeni kali ya serikali dhidi ya wapiganaji wa al-Shabab wanaodhibiti maeneo mengi ya kusini na katikati ya mji mkuu wa Mogadishu.Kundi hilo linajaribu kuitimua serikali ya Somalia likiwa na lengo la kuunda taifa linalozingatia sheria kali za kiislam.

XS
SM
MD
LG