Mapigano hayo yaliyofanyika katika wilaya ya Mangina, jirani na Beni, siku ya Jumatatu, jeshi limesema katika taarifa ya Jumanne.
Usalama umezorota tangu mwezi uliopita wakati mbunge katika bunge la jimbo akiwashawishi vijana wa kuchukua silaha, na kuanzisha kundi dogo la wanamgambo la kulipinga jeshi, taarifa kutoka kwa msemaji wa jeshi la eneo hilo Antony Mwalushayi ilisema.
Mbunge aliyetajwa katika taarifa, Alain Siwako alikanusha hili. Ameliambia shirika la habari la Reuters kwa njia ya simu kuwa wanamgambo wapiganaji hawakutoka Mangina na kuwa msemaji wa jeshi amemshutumu kwa sababu binafsi.
Siku ya Jumatatu wanajeshi waliokuwa katika doria walivamiwa na vijana wanamgambo, na kuwapiga risasi baada ya mapigano, ilisema taarifa ya shirika la habari la Reuters.
Mwandishi wa habari wa Reuters alihesabu miili saba ya raia katika mji huo siku ya Jumanne. Mkaazi mmoja alisema jirani yake alikuwa njiani kwenda kuifunga nyumba yake kabla ya kukimbia ndipo akapigwa risasi.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters
Forum