Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 06:14

Wanafunzi-Tanzania wasema wametimiza vigezo vya mkopo


Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Abdul Badru
Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Abdul Badru

Mamia ya wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu nchini Tanzania wamekusanyika katika Ofisi za Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu mjini Dar es Salaam kwa ajili ya kudai fedha za mikopo, huku vyuo mbalimbali vikiwa vimeanza masomo leo Jumatatu.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti kuwa makundi ya wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali wanaotarajiwa kujiunga na vyuo vya elimu walikusanyika kwa wingi huku wengine wakitoa vilio na malalmiko yao juu ya kukosa mikopo huku wakidai wametimiza vigezo vya kupata mikopo hiyo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:54 0:00


Baadhi ya wanafunzi wanadai kwamba wametimiza vigezo vilivyohitajika kwa ajili ya kupata malipo ya mikopo hiyo lakini hawajapata.

Wakizungumza na VOA wanafunzi hao wamesema sasa wamejikuta katika hali ya sintofahamu baada ya uongozi wa Bodi hiyo ya mikopo kuwapa majibu kuwa hawana sifa za kupewa mikopo.

Pia wamefahamishwa kuwa kutokana na kutotimiza vigezo vinavyotakiwa imewaathiri kwani tayari Usajili wa wanafunzi kwa baadhi ya vyuo umeanza na usajili huo unafanywa kwa kulipa nusu ya ada inayohitajika.

VOA imefanikiwa kuzungumza na uongozi wa Bodi ya Mikopo ya elimu ya juu Tanzania kuhusiana na malalamiko hayo ya uzuiaji wa mikopo kwa baadhi ya wanafunzi ambapo Meneja Mawasiliano Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania amekiri kuzuiliwa kwa mikopo kwa baadhi ya wanafunzi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutotimiza mmasharti na vigezo.

Pia ameahidi kushughuilikia malalamiko ya wanafunzi hao kwa kuzingatia masharti ya vigezo vilivyowekwa.

Vyanzo vya habari nchini Tanzania vimesema kuwa Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu tayari ametoa ufafanuzi kuhusu sifa na takwimu za utoaji mikopo kwa wanafunzi.

Serikali kupitia Rais John Magufuli Oktoba 27 mwaka huu ilisema tayari hazina imeidhinisha na kupeleka fedha kiasi cha shilingi bilioni 147 kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini huku rais akitahadharisha kutotaka kuona malalamiko ya wanafunzi waliokosa mikopo hiyo

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Tanzania

XS
SM
MD
LG