Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 05:05

Wamisri wakaidi amri ya serikali ya mpito


Wanawake wanaharakati wa kundi la kisiasa la kislamu Jamaat-e-Islami (JI) wanabeba picha za Mohamed Morsi wakati wa maandamano mjini Islamabad hapo August 18, 2013.
Wanawake wanaharakati wa kundi la kisiasa la kislamu Jamaat-e-Islami (JI) wanabeba picha za Mohamed Morsi wakati wa maandamano mjini Islamabad hapo August 18, 2013.
Mkuu wa jeshi la misri Jenerali Abdel-Fatah el-Sissi amesema jeshi halitoweza kukaa kimya inaposhuhudia ghasia baada ya mamia ya watu kuuliwa wakati wa ghasia za kisiasa za siku chache zilizopita.

Alizungumza wakati wafuasi wa rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi walikuwa wanaandamana kuelekea Mahakama Kuu ya Misri mjini Cairo.

Akizungumza na sauti ya Amerika kutoka Cairo mwanafunzi wa chuo kikuu cha Al-Azhar mjini cairo, Abdulrazak Niyigaba anasema tangu amri ya kutotoka nje kutangazwa wamisri wamekuwa wakikaidi na kuandamana usiku, Siku ya jumapili maandamano kutoka maeneo sita yalifanyika kuelekea mahakama ya katiba huku jeshi likiwazuilia watu kufika huko.
Mahojiano na a. Niyigaba
please wait

No media source currently available

0:00 0:05:34 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Wakati huo huo muungano wa makundi ya wanaharakati wa kislamu unaopinga kuondoelwa madarakani Bw. Morsi walifuta maandamano mawili yaliyopangwa hii jumapili wakidai walenga shabaha waliwekwa kwenye njia walopanga kupita.

Mkuu wa majeshi Jenerali el-Sissi akizungumza kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa ghasia za wiki iliyopita amesema jeshi halina nia yeyote ya kuchukua madaraka na akatoa wito kwa wanaharakati wa kislamu kujiunga na utaratibu wa kisiasa.

Umoja wa Ulaya, EU, umetanagza kwamba unatafakari juu ya uhusiano wake na Misri, wakati mawaziri wake watakapokutana jumatatu mjini Brussels kujadili maendeleo ya huko Misri.

Katika taarifa ndefu ya pamoja iliyotolewa jumapili na Baraza la Ulaya na Kamisheni ya Ulaya, inaeleza kwamba wito wa kupatikana demokrasia na kulinda haki msingi za binadamu hauwezi kupuuziwa, kadhalika kuoshwa na damu.

Wanaharakati wa kislamu na wandamanaji wengine wameandamana katika miji kadha ya Mashariki ya Kati na Asia.

Maelfu ya waarabu huko Israel walipepea bendera ya Misri na picha za Morsi jumamosi walipoandamana katika mji wa kaskazini wa Nazareth.

Maelfu ya watu walikusanyika Ankara na Istanbul Uturuki kuonesha uungaji mkono wao na waandamanaji wa Misri. Mkusanyiko mkubwa pia wa watu ulifanyika Indonesia na Malaysia kuihimiza serikali ya Msiri kuzuia kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji.

XS
SM
MD
LG