Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 08:59

Misri yatangaza amri ya dharura


Afisa wa usalama wa Misri anazungumza na mwanamke anaeshikilia mti katika kambi iliyoshmabuliwa na vikosi vya usalama. karibu na chuo kikuu cha Cairo huko Giza, Cairo, Misri, Jumatano
Serikali ya Misr imetangaza amri ya dharura kote nchini kuanzia hii leo, kwa muda wa mwezi moja kufuatana na taarifa ya rais iliyotangaza na televisheni ya taifa.

Taarifa hiyo ina liamrisha pia jeshi kukisaidia kikosi cha polisi "kutanzua mzozo unaotokea kote Misri."

Taarifa hiyo imetolewa wakati vikosi vya usalama vilikuwa vinashambulia makambi mawili kuwaondowa wafuasi wa rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi kati kati ya mji mkuu wa Cairo.

Wakati huo huo kumekuwepo na ripoti zinazotofautiana hii leo juu ya idadi ya watu walouliwa na walojeruhiwa katika ghasia zinazotokea kote nchini. Wizara ya afya inaeleza watu 95 wameuliwa na wengine 974 kujeruhiwa kote nchini.

hata hivyo baadhi ya wanachama wa chama cha Muslim Brotherhood cha Bw Morsi wanasema idadi ya walofariki imefikia hadi 2,200 na wengine elfu 10 kujeruhiwa. sauti ya amerika haijaweza kuthibitisha idadi hizo zote zinazotolewa.

XS
SM
MD
LG