Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 25, 2024 Local time: 11:21

Viongozi wa dunia walaani ghasia nchini Misri


Polisi wanamkamata mfuasi wa rais aliyepinduliwa Misri Mohamed Mursi wakati wa mapambano katikati ya Cairo Ogusati 13, 2013.
Polisi wanamkamata mfuasi wa rais aliyepinduliwa Misri Mohamed Mursi wakati wa mapambano katikati ya Cairo Ogusati 13, 2013.
Viongozi duniani Jumatano wamelaani vikosi vya usalama vya Misri baada ya kutumia nguvu na kusababisha vifo baada ya kutawanya wafuasi wa rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi.

Marekani pia inalaani vikali ghasia hizo.Katika taarifa, White House inasema ghasia hizo zitafanya iwe ngumu kwa Misri kusonga mbele kwenye njia ya kupata uthabiti na demokrasia ya kudumu.
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:14 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Katika mkutano na waandishi wa habari huko Martha’s Vineyard, Massachusetts ambako rais Obama na familia yake wapo mapumzikoni, naibu msemaji wa rais Josh Earnest alilaani ghasia hizo za Misri.

Alisema Washington inakariri mwito wake kwa jeshi na vikosi vya usalama vya Misri kuonyesha ustahmilifu na kuheshimu haki za msingi za binadamu kwa raia wa Misri, huku pia wakiwasihi waandamanaji kuandamana kwa amani.

“Pia tunapinga vikali hatua ya kurejea kwa uhali ya dharura nchini humo na tunatoa wito kwa serikali kuheshimu haki za msingi za binadamu kama vile uhuru wa mkusanyiko kwa amani kwa mujibu wa sheria. Dunia inaangalia kile kinachotokea mjini Cairo. Tunaisihi serikali ya Misri na vyama vyote nchini humo kujiepusha na ghasia na kutatua tofauti zao kwa amani”

Rais Obama hivi sasa anakabiliwa na masuala yale yale kuhusu namna anavyokabiliana na hali nchini Misri na maelezo juu ya namna rais Morsi alivyoondoka madarakani mwezi Julai.

Utawala wa Washington ulikataa kuchukua msimamo kwamba yalifanyika mapinduzi nchini humo. Chini ya sheria ya Marekani hilo litahitajika kusitisha msaada wa dola bilioni 1.5 zinazotolewa na Marekani kwa ajili ya uchumi na jeshi la Misri.

Miongoni mwa viongozi walolaani ghasia za jana Cairo ni Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ambaye chama chake kina ushirika wa karibu na chama cha Muslim Brotherhood, alilaani kile alichokieleza kuwa mauaji ya halaiki na kuisihi Umoja wa mataifa kufanya uchunguzi.

Waziri wa mambo ya nje wa uingereza William Hague alisema katika taarifa kuwa “ninalaani utumiaji wa nguvu katika kuwatawanya waandamanaji na kutoa wito kwa majeshi ya usalama kuchukua hatua za kujiepusha na ghasia”.

Mataifa ya ulaya pia yalihisihi serikali ya Misri na wapinzani wake chama cha ki-Islam kuepuka kuongezeka kwa ghasia na kurudi kwenye mashauriano ya kisiasa.

Masemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki-Moon alisema mkuu wa Umoja wa mataifa analaani ghasia nchini Misri na anasikitika kwamba maafisa wa Misri walichagua kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji wengi wao wanaharakati wa ki-islam.

Kundi la kutetea haki za binadamu la Amnesty international linalitaka jeshi la Misri kuacha kuwashambulia waandamanaji.
XS
SM
MD
LG