Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 09, 2023 Local time: 12:39

Wamarekani wachukua tahadhari kutokana na ilani iliyotolewa kwa wasafari


Wasafiri wakiwa uwanja wa ndege wa kimataifa Ronald Reagan, Washington, DC
Wasafiri wakiwa uwanja wa ndege wa kimataifa Ronald Reagan, Washington, DC

Hali ya hewa mbaya kote nchini  Marekani na Canada imepelekea watu zaidi ya milioni 135 kuwa katika tahadhari ya hali ya hewa kabla ya shughuli nyingi za kusafiri mwishoni mwa mwaka.

Tahadhari hizo zimeenea kutoka pwani hadi pwani na kufika kusini kabisa mwa mpaka wa Marekani na Mexico na Florida katika jimbo la Sunshine.

Viwanja vya ndege vikubwa vimefuta safari zake wakati dhoruba ikizidi kuwa mbaya.

Wakati dhoruba ikipiga eneo la maziwa makuu Alhamisi hali ya hewa ambayo inajulikana kama kimbunga bomu kilikuwa kinatarajiwa kushika kasi kwa katika shinikizo la chini linaloongezeka zaidi , huduma ya kitaifa ya hali ya hewa NWS imesema.

Kimbunga hicho kinaweza kusababisha kunyesha kwa theluji hadi nusu inchi kwa saa huku kukiwa na upepo unaovuma kutoka nyanda za juu za Magharibi Kati hadi eneo la Kaskaizini Mashariki na kusababisha upeo wa kuona ukawa karibu sifuri , idara ya hali ya hewa imesema.

Inawezekana umeme ukakatika kutokana na dhoruba yenye upepo mkali , theluji nyingi na barafu, ukichanganya na mahitaji makubwa ya nishati na dhoruba ilitarajiwa kusababisha baadhi ya nyakati usafiri kuwa wa shida.

XS
SM
MD
LG