Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 11:12

Safari za ndege zaidi zafutwa kutokana na COVID-19


Wasafiri wakifuatilia taarifa za safari za ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Los Angeles, California, Disemba 24, 2021.(Photo by DAVID MCNEW / AFP).
Wasafiri wakifuatilia taarifa za safari za ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Los Angeles, California, Disemba 24, 2021.(Photo by DAVID MCNEW / AFP).

Kumekuwepo na matukio zaidi ya kufuta safari za ndege yaliyohusishwa na kesi za COVID -19 wakati wiki inaanza na kuvuruga sikukuu kwa maelfu ya watu.

Zaidi ya ndege 1,400 safari zake zimefutwa Jumatatu, huku vituo vya Marekani na China vikiwa vimepigwa vibaya, tovuti inayofuatilia data za safari za ndege imesema.

Mashirika ya ndege ya Marekani yamesema kuvurugwa kwa safari za ndege kumetokana na wafanyakazi kupimwa na kukutwa na Corona au kutakiwa kujitenga.

Hong Kong imepiga marufuku safari zote za ndege za Korea Kusini kwa wiki mbili baada ya kutokea kesi za corona kwa watu waliowasili.

Zaidi ya ndege 800 zimezuiliwa mwishoni mwa wiki wakati wa sikukuu ya Krismas iliyoanza Ijumaa iliyopita.

ingawa idadi ya kufuta safari za ndege ni asilimia ndogo lakini ni kubwa kuliko kawaida na imekuja wakati wa kipindi cha mwaka ambapo watu wengi wanasafiri kutumia muda wao na familia na marafiki.

Wakati huohuo maafisa wa Marekani wanafuatilia dazeni za meli zilizokumbwa na kesi za COVID-19 wakati zikiwasili katika eneo la maji ya Marekani kukiwa na baadhi ambazo zilizokataliwa katika bandari ya Caribbean, shirika la Habari la AFP limesema.

Kesi za COVID-19 zilizoandikishwa zinaongezeka kote ulimwenguni nyingi zikitokana na kirusi cha Omicron.

XS
SM
MD
LG