Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 09, 2023 Local time: 11:51

Johns Hopkins : Vifo vyafikia zaidi ya laki nane vya COVID-19 Marekani


 Kidonge cha COVID-19, Paxlovid cha kampuni ya Pfizer kilichotangazwa Oktoba 2021.(Pfizer via AP)V
Kidonge cha COVID-19, Paxlovid cha kampuni ya Pfizer kilichotangazwa Oktoba 2021.(Pfizer via AP)V

Idadi ya kesi zilizothibitishwa Marekani za COVID 19 zimeongezeka kufikia zaidi ya milioni 50 hadi Jumatano huku kukiwa na idadi ya vifo zaidi ya laki nane kwa mujibu wa data zilizotolewa na taasisi ya sayansi ya chuo kikuu cha Johns Hopkins.

Kesi za COVID -19 za wastani wa siku saba nchini zimeongezeka kwa asilimia 25 kutoka wiki iliyopita karibu kesi 149,300 kwa siku kukiwa na vifo kwa siku vya asilimia 3.5. kituo cha kudhibiti na kuzuiya magonjwa cha CDC kimesema Jumatano.

Maabukizo ya kirusi cha Omicron yanawakilisha asilimia 73 ya kesi kote nchini , CDC imesema.

Wakati huohuo wakaguzi wa masuala ya afya Marekani wamepitisha kidonge cha kwanza cha COVID -19, kilichotengenezwa na kampuni ya Pfizer ambacho wamarekani wanaweza kukitumia nyumbani kwa ajili ya matokeo mabaya ya maambukizi ya kirusi.

Hatua hiyo iliyosubiriwa kwa muda mrefu imekuja wakati ambapo kesi hapa Marekani, kulazwa hospitali na vifo vinaongezeka na maafisa wa afya wameonya maambukizo mapya yanayotokea kutokana na kirusi cha Omicron yanaweza kuzifanya hospitali kuelemewa zaidi. dawa hiyo inayoitwa Paxlovid ni njia ya haraka kutibu COVID -19.

Jeff Zients, Mratibu wa White House wa COVID -19: “ikijulikana kwamba kidonge hicho kinachukua muda kutengenezwa, Pfizer inaendelea kuongeza mipango ya uzalishaji, na sasa kwa sababu kidonge kimethibitishwa tutakuwa na majadiliano kuona ni jinsi gani ya kuwasaidia ili kuboresha uzalishaji wao kwa haraka kwa kuwapatia rasilimali zinazohitajika.

Tutakuwa na tiba 265,000 mwezi Januari, na idadi ya vidonge kwa mwezi vitakavyotolewa kwa mwaka mzima na tiba zote milioni 10 zitatolewa ifikapo majira ya joto. Kwa haraka Pfizer itakapotengeneza vidonge na kusambaza tutavitoa haraka Katika majimbo kwa ajili ya kusambaza.”

XS
SM
MD
LG