Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 06, 2023 Local time: 19:31

Waliosalia Khartoum wakabiliwa na uhaba wa chakula, maji na mawasiliano hafifu


Watu wakiwa wamebeba mali zao, wakitembea kando kando ya barabara huko Khartoum, tarehe 16 Aprili 2023. Picha na Shirika la habari la AFP.

Mapigano yamepamba moto Jumatano katika mji mkuu wa Sudan na mji ulio wa kusini, wakazi walisema hali hiyo imewasukuma watu wengi kufanya safari hatari kuelekea maeneo salama kuvuka mipaka ya nchi.

Wale ambao wameshindwa kuondoka wanakabiliana na uhaba wa chakula na huduma nyingine muhimu, kitu pekee nchini humo kinachowasaidia ni mitandao ya misaada miongoni mwa marafiki na majirani, wakati mazungumzo ya kuwezesha ufikishaji salama wa misaada hayaonyeshi dalili ya kusonga mbele.

"Tuliamshwa na milipuko na mizinga mikubwa iliyokuwa ikifyatuliwa," mkazi mmoja wa Omdurman, mji wenye uhusiano na Khartoum aliliambia shirika la habari la AFP wakati moshi ukifuka kwenye mji huo mkuu.

Wakati wa usiku, milipuko miwili mikubwa ilisikika sehemu kubwa ya mji wa Khartoum, wakazi wa wilaya mbalimbali walisema, Hii ni wiki ya nne tangu vita vianze kati ya mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na aliyekuwa makamu wake Mohamed Hamdan Daglo ambaye anaongoza Kikosi cha Rapid Support Forces (RSF).

Pia wakazi wa El Obeid, mji mkuu wa jimbo la Kordofan Kaskazini, uliopo takriban kilomita 350, kusini magharibi mwa Khartoum waliripoti mapigano na milipuko siku ya Jumatano.

Tangu mapigano yazuke Sudan tarehe 15 Aprili, mkazi wa Khartoum Omar amesema yeye na baba yake hawajaondoka nyumbani kwao na wanaamini kuwa ni raia pekee waliosalia katika kitongoji hicho.

Wamejiwekea kikomo kwa mlo mmoja kwa siku, wakitumaini kiwango kidogo cha chakula walichonacho kitadumu kwa mwezi zaidi ya mmoja. "Baada ya hapo, hatujui tutafanya nini, mbali na kujinusuru kwa maji na tende," alisema kwa njia ya simu kutoka mji mkuu huo wa Sudan unaokabiliwa na mgogoro.

Wakati maelfu ya watu wameukimbia mji huo mkuu - ambao kabla ya vita ya ulikuwa na watu milioni 10 - wengi wao wamesalia, baadhi yao wameshindwa kuondoka kwa kuwa ni hatari sana au gharama kubwa za kuondokea, wakati wengine wakinga’g’ania kwenye nyumba zao.

Waliosalia wanakabiliwa na uhaba wa chakula, umeme maji na mawasiliano hafifu ya simu. Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu janga kubwa la kibinadamu, umesema unafanya kazi ili kuwepo na makubaliano yaitakayowezesha Khartoum kufikiwa na misaada kwa usalama.

Chanzo cha habari hii ni mashirika ya habari ya AFP na Reuters

XS
SM
MD
LG