Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 22, 2025 Local time: 12:35

Walinda Amani wa UN waamriwa kuondoka Mali haraka


Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, MUNISMA wakifanya doria katika mitaa ya Gao, Mashariki mwa Mali Agosti 3, 2018. Picha na SEYLLOU / AFP.
Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, MUNISMA wakifanya doria katika mitaa ya Gao, Mashariki mwa Mali Agosti 3, 2018. Picha na SEYLLOU / AFP.

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa, wameamriwa kuondoka nchini Mali na viongozi wa nchi hiyo, wametakiwa kuondoka haraka, na hivyo kuharibu vifaa vilivyobaki nyuma, na kuhatarisha maisha yao wakiwa njiani, wanaharakati walisema Ijumaa.

Kufuatia mapinduzi ya mwaka 2020 watawala wapya wa kijeshi mwezi Juni waliwaamuru walinda amani kuondoka, wakitangaza "kushindwa" kwa misheni yao na kukemea madai ya "utumiaji" wa suala la haki za binadamu kutimiza malengo yao.

Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Utulivu nchini Mali (MINUSMA), ambacho kina nguvu za wanajeshi takriban 15,000 na maafisa wa polisi, kimeshuhudia wanajeshi 180 kati yao wakiuawa.

Mpango wa awali ulikuwa kikosi cha kulinda amani kiwe kimeondoka katika taifa hilo la Afrika Magharibi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, lakini tayari wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wamekuwa wakiondoka kwenye kambi zao moja baada ya nyingine, na kwa mara ya kwanza waliweza kuondoka mwanzoni mwa mwezi Julai.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG