Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 27, 2025 Local time: 13:28

Mali yachunguza ombi la shirika la ndege la Ufaransa la kurejesha safari zake


Ndege za shirika la ndege la Ufaransa zikiwa imeegeshwa katika uwanjwa wa ndege wa Paris Charles de Gaulle huko Roissy Aprili 30, 2020. Picha na BERTRAND GUAY / AFP.
Ndege za shirika la ndege la Ufaransa zikiwa imeegeshwa katika uwanjwa wa ndege wa Paris Charles de Gaulle huko Roissy Aprili 30, 2020. Picha na BERTRAND GUAY / AFP.

Wizara ya uchukuzi ya Mali ilisema Jumatano imekuwa ikilichunguza ombi la shirika la ndege la Ufaransa kuanza tena safari za kwenda na kutoka mji mkuu Bamako, wakati huo huo safari hizo za ndege zimesimamishwa.

Utawala wa Kijeshi wa Mali imefuta idhini iliyotolewa kwa Air France kuanza tena safari za ndege kwenda nchini humo, maafisa wawili waandamizi na afisa wa usafiri wa anga walisema Jumatano.

Tangazo hilo limekuja siku moja baada ya Air France kutangaza kurejesha safari zake kuanzia Ijumaa baada ya kusimamisha tangu Agosti 7 kufuatia mapinduzi katika nchi jirani ya Niger.

“Uamuzi huo umeakhirishwa kwa sababu makubaliano hayo yalitolewa bila kushauriana na uongozi,” alisema ofisa mmoja.

Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, afisa huyo ameongeza kuwa mkurugenzi wa usafiri wa anga wa Mali amefutwa kazi, bila ya kusema amefukuzwa kwa misingi gani.

"Hakutakuwa na ndege za shirika la ndege siku ya Ijumaa," afisa mwingine alisema. "Hili lazima lifanyike kwa njia ya uwajibikaji na iliyoratibiwa, wakati wote tukiheshimu uhuru wetu".

Afisa wa usafiri wa anga alithibitisha kuwa "idhini imefutwa", bila kutoa maelezo zaidi.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP na Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG