Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 22, 2025 Local time: 08:34

Putin afanya mazungumzo na kiongozi wa Mali


Rais wa Russia, Vladimir Putin afanya mzungumzo ya biashara na usalama na kiongozi wa Mali, Jumanne.

Mazungumzo hayo ni ya tatu ya simu katika muda wa chini ya miezi miwili, Kremlin imesema.

Mara kwa mara mawasiliano ya rais Putin na rais wa mpito wa Mali, Assimi Goita, yanajikita katika nia kubwa ya Moscow, kukuza ushawishi wake katika kanda inayokabiliwa na mapinduzi ya Sahel, Afrika Magharibi kiujumla.

Russia inaongeza uhusiano wa kiusalama kwa kuzidi kuyatenga mataifa ya Ufaransa na Marekani.

Viongozi hao wawili walijadili dhamira yao ya pamoja ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi, ushirikiano wa kiusalama na mapambano dhidi ya ugaidi,” ilisema taarifa ya Kremlin.

Rais Goita, aliandika kwenye mtandao wa kijamii akisema, “natoa shukrani zangu kwa msaada wote ambao Russia, inatoa kwa Mali.”

Forum

XS
SM
MD
LG