Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:55

Wakuu wa usalama wawataka waandamanaji kufuata sheria


Wanajeshi wakilinda doria nje ya Shopping Mall huko Vosloorus, mashariki ya Johannesburg, South Africa, July 14, 2021.
Wanajeshi wakilinda doria nje ya Shopping Mall huko Vosloorus, mashariki ya Johannesburg, South Africa, July 14, 2021.

Wakuu wa usalama nchini Afrika Kusini, wametoa wito wa kusitishwa ghasia baada ya watu zaidi ya 100 kukamatwa Jumanne kuhusiana na uporaji baada ya ghasia kuzuka kufuatia kufungwa jela kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Jacob Zuma.

Waziri wa Polisi wa nchi hiyo, Bheki Cele, alisema vikosi vya usalama havitakubali kile alichokiita ‘kejeli kwa serikali yetu ya kidemokrasia,” na wataongeza juhudi maradufu, kukomesha ghasia hizo.

Waziri wa Polisi wa Afrika Kusini ameeleza : "Hakuna hali yoyote ya kutokuwa na furaha au ya masuala binafsi yanayompa mtu yeyote haki ya kupora, kuharibu na kufanya apendavyo, na kuvunja sheria. Tunatoa wito kwa jamii kujizuia katika kushughulikia hali hiyo, na juu ya yote, kuhakikisha kuwa raia wasio na hatia hawaumizwi. Tunazidi kuwasihi watu wote kukataa wito wowote wa vurugu, na kufanya iwe vigumu kuitawala nchi. "

Wakati uporaji ulipoanza katika mji mkuu wa kiuchumi wa Johannesburg, na jimbo la kusini mashariki la KwaZulu-Natal, upinzani mkuu wa Afrika Kusini, uliwashutumu watu wenye msimamo mkali, kwa kusababisha machafuko.

Uharibifu uliofanywa na watu waliopora mali katika maduka ya Jabulani mall, wanajeshi wapelekwa kuzuia ghasia, wizi na uharibifu wa mali za Umma.
Uharibifu uliofanywa na watu waliopora mali katika maduka ya Jabulani mall, wanajeshi wapelekwa kuzuia ghasia, wizi na uharibifu wa mali za Umma.

Watu wengi kote nchini wanasafisha au kulinda biashara zao baadhi wakihisi kwamba hawajasaidiwa vya kutosha.

Afrika Kusini imeshuhudia uporaji mkubwa wa biashara, na machafuko tangu tarehe 9 mwezi Julia, na angalau watu 72 wamefariki, kulingana na idadi rasmi iliyotolewa na serikali.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma

Zuma anatumika kifungo cha miezi kumi na tano gerezani kwa kuidharau mahakama.

XS
SM
MD
LG