Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 13:44

Ghasia zaendelea Afrika kusini


Mwanajeshi ashika doria Afrika kusini
Mwanajeshi ashika doria Afrika kusini

Maduka na maghala nchini Afrika kusini yameporwa Jumanne kwa siku ya tano mfululizo, licha ya hatua ya rais Cyril Ramaphosa kupeleka wanajeshi mitaani ili kuzima kudhibiti hali.

Ghasia tayari zimesababisha vifo vya watu 45. Wakati uporaji mkubwa ukifanyika kwenye mji mkuu wa kiuchumi wa Johannesburg pamoja na jimbo la kusini mashariki la KwaZulu Natal.

Mzozo umezuka kwenye uwanja wa kisiasa, ambapo wapinzani wakuu wa Afrika kusini wanawashtumu watu wenye msimamo mkali kwa kuchochea ghasia. Wanajeshi elfu 2,500 wamepelekwa kusaidia polisi, waliokua wamezidiwa.

Lakini idadi hiyo ni ndogo sana ikilinganishwa na zaidi ya wanajeshi elfu 70 waliopelekwa kwenye mitaa mwaka jana, ili kusaidia kuimarisha masharti makali ya kupambana na janga la corona.

Jumanne, idadi ndogo ya wanajeshi walionekana kwenye baadhi ya vituo vya biashara. Ghasia zilizuka kwa mara ya kwanza ijumaa iliyopita baada ya rais wa zamani Jacob Zuma kuanza kutumikia kifungo cha miezi 15 jela, hatia kudharau mahakama.

Mwishoni mwa juma, ghasia zilienea katika jimbo la Gauteng ambalo linajumuisha mji wa Johannesburg, ambako miili 10 ilipatikana Jumatatu kwenye kitongoji cha Soweto.

XS
SM
MD
LG