Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 25, 2020 Local time: 19:46

Wahindu- India wapinga hatua iliyo chukuliwa na serikali


Wanawake wakila kiapo kupinga ubaguzi wa kijinsia Kusini mwa jimbo la Kerala, India Jumanne, Januari. 1, 2019. (AP Photo/R.S. Iyer)

Makundi yenye msimamo mkali kutoka jamii ya Wahindu nchini India, yamesababisha shughuli kukwama katika mji wa Kerala na majimbo yaliyo karibu, katika maandamano ya kupinga hatua ya serikali ya kuwaruhusu wanawake wawili kuingia katika hekalu.

Uamuzi huo wa kuwaruhusu wanawake kuingia ndani ya hekalu unakaidi katazo la mila ya Wahindu ya kupiga marufuku wanawake kuingia katika eneo hilo.

Takriban waandamanaji 400, wakiwemo wanawake wameandamana kwenye barabara za Kochi, katika mji wenye shughuli nyingi za kibiashara wa Kerala, wakiongozwa na chama cha Waziri Mkuu Narendra Modi cha Bharatiya Janata – BJP na kile cha Rashtriya Swaya-msevak Sangh -RSS), chama kikongwe kabla ya BJP.

Maduka yamefungwa, na shughuli za usafiri kusitishwa, madereva wakieleza hofu ya kushambuliwa iwapo wangebeba abiria.

Mahakama ya juu ya India, mwezi septemba, ilifutilia mbali marufuku ya kutowaruhusu wanawake waliobalekhe kuingia katika hekalu la mlima Sabarimala, ambalo huvutia mamilioni ya waumini kila mwaka.

Facebook Forum

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG