Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 11, 2024 Local time: 05:53

Polisi India wakamata Wakatoliki wakifanya ibada za Krismas


Waziri Mkuu wa India Narendra Modi
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi

Polisi nchini India wamewakamata dazeni ya waumini wa Kikatoliki wakiimba nyimbo za Krismas kwa madai ya kuwa walikuwa wanajaribu kuwaingiza watu katika Ukristo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP Maafisa hao wa polisi wamesema Ijumaa, wakati hofu ikiongezeka juu kukandamizwa kwa uhuru wa kuabudu katika taifa hilo lilioko kusini mwa Asia.

Polisi wamesema watu 32 wametiwa nguvuni kwa kujaribu kuwaingiza watu katika Ukristo katika mji ulioko kati nchini India, Madhya Pradesh, jioni Alhamisi, wakati kiongozi wa umoja wa Wakatoliki akilaani tuhuma hizo na kusema “zinachekesha”.

Wakati kundi la wachungaji walipokwenda kituo cha polisi kuulizia kuhusu kukamatwa watu hao, gari lao lililokuwa limeegeshwa lilichomwa moto, ikidaiwa uchomaji huo umefanywa na kikundi cha mrengo wa kulia cha Wahindu, amesema Theodore Mascarenhas, katibu mkuu wa Umoja wa Maaskofu wa Kanisa Katoliki India.

Habari hizi zimetolewa wakati Wahindi Wakristo waliowachache wamekuwa wakilalamika kufuatia wimbi la mashambulizi katika makanisa na waumini wake, wakilaumu vitendo hivyo vya uvunjifu wa amani kuwa vinafanywa na Wahindu wenye msimamo mkali, ambao wamepata nguvu tangia Waziri Mkuu wa nchi hiyo Narendra Modi alipochukua madaraka mwaka 2014.

Mascarenhas amesema Wakatoliki 32 wakiwemo wachungaji wawili, walitiwa nguvuni wakati “wakiendesha programu ya nyimbo za ibada ya Krismas”.

Amesema kuwa ibada hiyo ya Carol imekuwa ni sehemu ya msimu wa Krismas katika eneo la Satna “ kwa miaka 30 sasa.”

XS
SM
MD
LG