Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 25, 2024 Local time: 16:48

Wahamiaji wasio na vibali vya ukaazi wanafanya mgomo wa kula huko Ubelgiji


Wauguzi wakiwapeleka hospitali wahamiaji waliogoma kula huko Ubelgiji. June 2, 2021.
Wauguzi wakiwapeleka hospitali wahamiaji waliogoma kula huko Ubelgiji. June 2, 2021.

Wanaume wapatao 450 hasa kutoka Morocco na Algeria wamekuwa wakifanya mgomo huo katika maeneo matatu ya Brussels tangu mwisho wa Mei wakitaka serikali iwape haki ya kubaki baada ya miaka kadhaa ya kufanya kazi nchini humo bila vibali

Hali ya Hofu iliongezeka Jumatatu mjini Brussels huko Ubelgiji kutokana na afya ya mamia ya wahamiaji wasio na hati maalum za ukaazi nchini humo baada ya kuendelea na mgomo wao wa njaa wenye lengo la kuwataka maafisa wa uhamiaji kuwaruhusu kubaki nchini humo.

Wanaume wapatao 450 hasa kutoka Morocco na Algeria wamekuwa wakifanya mgomo huo katika maeneo matatu ya Brussels tangu mwisho wa Mei wakitaka serikali iwape haki ya kubaki baada ya miaka kadhaa ya kufanya kazi nchini humo bila vibali.

Wafanyakazi wa afya wamesema kwamba watu 300 wanaogoma sasa wameanza kukataa kula kitu chochote wakijaribu kuongeza shinikizo lao. Wakuu wa vyama vya Kisoshalisti na Kijani, wanachama wa muungano unaotawala Ubelgiji katika taarifa yao mwishoni mwa wiki walionya kwamba janga lipo karibu na mauti yanawakaribia wanaogoma.

Maafisa hadi sasa wamesisitiza kwamba hawatakipa kikundi chochote cha wanaodai haki ya kukaa nchini humo licha ya kuongezeka kwa wito wa kupata suluhisho la haraka.

Nembo ya Umoja wa Mataifa (UN)
Nembo ya Umoja wa Mataifa (UN)

Wawakilishi wawili maalum wa Umoja wa Mataifa waliandika barua ya wazi kwa waziri wa uhamiaji wa Ubelgiji wakiwataka maafisa kuondoa tishio lolote la kuwaondowa nchini kwa sababu za kiafya na wafikirie kutoa vibali vya makazi vya muda mfupi.

Madaktari wa kundi la hisani la Doctors of the World waliviambia vyombo vya habari vya mji huo kuwa wanahofia kuwa wanaofanya mgomo wa chakula wako katika hatari ya kupata mshtuko wa ghafla wa moyo kwani hali yao ya mwili imekuwa dhaifu sana.

XS
SM
MD
LG