Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 23:25

Wafanyakazi washeherekea kuanza safari za ndege za South African Airways


Ndege ya Shirika la ndege la South African Airways
Ndege ya Shirika la ndege la South African Airways

Wafanyakazi waliokuwa na furaha kubwa wa shirika la ndege la Afrika Kusini, South African Airways, waliimba na kucheza wakati ndege ziliporuka kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha karibu mwaka mmoja.

Shirika hilo la ndege linalomilikiwa na serikali lilikuwa na matatizo makubwa ya kifedha kwa muda mrefu kutokana na janga la virusi vya Corona.

Kutokana na COVID-19 shirika la ndege hilo lilisitisha operesheni zake Septemba mwaka 2020, wakati lilipoishiwa na fedha.

Kampuni hiyo mwezi April iliishukuru serikali kwa kuipa fedha za kujikwamua kiuchumi.

Shirika hilo pia limeanza kufanya safari za ndani kutoka Johannesburg hadi CapeTown leo na wiki ijayo litaanzisha taratibu safari za kimataifa kwenye miji mikuu mitano ya Afrika.

Miji hiyo ni Pamoja na Accra, Kinshasa, Harare, Lusaka na Maputo.

Serikali ilisema itauza hisa kubwa za SAA kwa wadau wa ndani na utaratibu wa awali umeshakamilika.

XS
SM
MD
LG