Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:06

Wafanyakazi 3 wa afya wauawa katika vituo vya Ebola mashariki mwa DRC


Shirika la Madaktari wasiokuwa na mipaka (MSF) wakitoa chanjo ya Ebola katika Kituo cha Goma Nov. 14, 2019.
Shirika la Madaktari wasiokuwa na mipaka (MSF) wakitoa chanjo ya Ebola katika Kituo cha Goma Nov. 14, 2019.

Wafanyakazi watatu wa afya wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanyika katika vituo viwili vya kupambana na Ebola huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) mapema Alhamisi.

Hayo yameelezwa na maafisa wa afya wakati ghasia na vurugu kwa kiasi kikubwa zimedumaza juhudi za kuudhibiti mlipuko wa pili wa Ebola ambao umeuwa watu 2,199 tangu ulipozuka Agosti mwaka 2018.

Wanamgambo wa ndani wanaojulikana kama Mai Mai wanarudia kushambulia vituo vya afya kwa sababu wanaamini Ebola haipo na kwamba majibu yake ni njama ya kutokomeza idadi ya watu kwenye eneo hilo.

Wanamgambo wa Mai Mai mara kwa mara wanashambulia vituo vinavyotoa matibabu ya Ebola huko Mangina katika eneo la Kivu kaskazini na Byakoto huko Ituri, alisema Jean-jacques Muyembe, mkuu katika kitengo cha majibu ya Ebola huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC.

XS
SM
MD
LG