Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:41

Raia 14 wameuwawa na wengine kujeruhiwa huko Ituri kaskazini mashariki mwa Congo


Mashambulizi huko Ituri yamesababisha vifo na watu wengine kujeruhiwa
Mashambulizi huko Ituri yamesababisha vifo na watu wengine kujeruhiwa

Mwezi Juni, watu 160 waliuwawa katika jimbo hilo la Ituri na zaidi ya watu 300,000 walikimbia ghasia zilizosababishwa na wanamgambo wa jimbo hilo kulingana na taarifa ya kiongozi wa kijamii kwenye jimbo, Desire Malo

Raia 14 waliuwawa na wane walijeruhiwa siku ya Jumatano katika shambulizi moja la wanamgambo katika jimbo la kaskazini mashariki la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC ambako kumekuwepo na ghasia kwa miezi kadhaa.

Mwezi Juni, watu 160 waliuwawa katika jimbo hilo la Ituri na zaidi ya watu 300,000 walikimbia ghasia zilizosababishwa na wanamgambo wa jimbo hilo kulingana na taarifa ya kiongozi wa kijamii kwenye jimbo, Desire Malo ambaye aliliambia shirika la habari la AFP.

Wakati huo huo kiongozi wa wilaya ya Djugu alithibitisha idadi ya vifo hivyo akisema wanamatumaini kuwa jeshi litachukua tahadhari zote kulinda raia. Naye msemaji wa jeshi katika jimbo Jules Tshikudi alisema walikuwa wakiendelea kuwasaka washambuliaji ambao wamewashambulia watu wasio na hatia.

Mwishoni mwa mwaka 2017 na mwanzoni mwa mwaka jana wilaya ya Djugu katika jimbo la Ituri ilikumbwa na mapigano ya kikabila yaliyosababisha darzeni ya vifo na maelfu walikimbia kukatisha mpaka na kuingia nchini Uganda.

XS
SM
MD
LG