Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 21, 2024 Local time: 05:46

Waendesha bodaboda 3 Kenya wauawa na al-Shabaab


Wapiganaji wa al-Shabaab bado waendelea kufanya mashambulizi ya kinyama nchini Kenya.
Wapiganaji wa al-Shabaab bado waendelea kufanya mashambulizi ya kinyama nchini Kenya.

Waendesha pikipiki watatu, maarufu kwa jina la bodaboda, wameuawa na shambulizi linaloshukiwa limefanywa na al-Shabaab katika eneo la Witu, kwenye Kaunti ya Lamu, Kenya.

Watu hao watatu walikufa baada ya mtu mwenye silaha kurusha risasi kwenye basi na gari la kampuni ya ulinzi lililokuwa linaelekea huko eneo la Kipini kutoka mji wa Malindi.

Washambuliaji hao walilitupia risasi basi ambalo ni mali ya kampuni ya Kipini Raha katika barabara kuu ya Garsen-Lamu katika mida ya saa 3.30pm, kwa mujibu walioshuhudia tukio hilo..

Wapiganaji hao walitupa risasi kila upande kutoka porini kabla ya polisi waliokuwa wanalisindikiza gari hilo kuja haraka kuwaokoa watu waliokuwa wanasafiri katika basi hilo.

Vyanzo vya habari vimesema kuwa kuna wasafiri ambao idadi yao haijajulikana waliokuwa wamejeruhiwa na walipelekwa hospitali ya Kaunti ndogo huko Witu.

Mkurugenzi Joseph Kanyiri aliyechaguliwa kusimamia operesheni hiyo ya Linda Boni amethibitsha kutokea shambulizi hilo lakini amesema bado anasubiri taarifa zaidi juu ya shambulizi hilo.

XS
SM
MD
LG