Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 12:21

Wademokrat wadai Warepublikan wamebadilisha waraka wa siri


Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Devin Nunes
Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Devin Nunes

Mdemokrat wa ngazi ya juu katika Kamati ya Usalama ya Bunge la Marekani amesema Jumatano Warepublikan katika kamati hiyo wamebadilisha waraka wa siri.

Amedai kuwa ulibadilishwa kabla ya Warepublikan kuutuma ikulu ya White House, na wala hawakuupeleka waraka ambao waliuonyesha kwa wabunge na kupitishwa katika kura iliyopigwa na vyama hivyo kwa mujibu wa msimamo wa vyama vyao.

Waraka huo, ambao ikulu ya White House wanaweza kuamua kusambaza kwa umma mapema kabisa Alhamisi, inadaiwa unaonyesha kuikandamiza Idara ya Sheria kwa kuionyesha iko dhidi ya Rais Donald Trump.

Mbunge Adam Schiff amesema katika barua alioituma kwa Mwenyekiti wa kamati Devin Nunes kuwa Wademokrati waligundua Jumatano jioni kwamba waraka huo ulikuwa umefanyiwa “mabadiliko makubwa” na wanakamati walishindwa kupitia waraka huo au kuupitisha, na hali hiyo ilikuwa “inatatiza sana.”

Wakati mabadiliko ya upande wa waliowengi haujasahihisha upotoshaji na makosa katika waraka wako, lakini bado hayo yatakuwa na athari,” Schiff amesema.

Msemaji wa Nunes ametoa tamko kueleza kwamba waraka uliotumwa ikulu ya White House ilikuwa na “marekebisho machache” na Wademokrat walikuwa wanajaribu kuzuilia “dosari zilizoelezwa katika waraka huo.”

"Katika jitihada inayoendelea kushangaza kujaribu kuzuia kutolewa kwa waraka huo, wanakamati waliowachache wanalalamika juu ya marekebisho machache yaliyofanywa katika waraka huo, yakiwemo marekebisho ya msamiati na marekebisho mawili yaliyoombwa Shirika la Upelelezi (FBI) na upande wa waliowachache," msemaji huyo ameeleza.

Mapema Jumatano, Idara ya Upelelezi ya Serikali kuu imesema ina “mashaka makubwa” juu ya usahihi wa waraka huo na ilikuwa na “fursa finyu sana” kupitia waraka huo wa kurasa nne kabla ya kamati kupiga kura kuidhinisha kutolewa kwa umma.

Nunes amesema kupinga kwa FBI juu ya waraka huuni “uzushi.”

XS
SM
MD
LG