Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 03, 2022 Local time: 01:46

Wabunge wa Republikan wapata ajali


Eneo lilipotokea ajali ya treni, Virginia

Treni iliokuwa imewabeba wabunge wa chama cha Republikan kutoka mjini Washington wakielekea upande wa Virginia Magharibi kwenye mkutano iligongana na gari aina ya lori Jumatano huko kusini magharibi ya Virginia, na kuuwa mtu mmoja aliyekuwa katika lori.

Ikulu ya White House imesema hakuna mbunge yoyote au wasaidizi wao ambao walipata majeraha mabaya.

Tamko limesema, “Kuna mtu mmoja ameuwawa na mwengine amepata majeraha mabaya. Hakuna majeruhi ya kutisha kwa upande wa wabunge na wasaidizi wao. …Maombi yetu na fikra zetu zote ziko pamoja na walioathirika na ajali hii.”

Ajali hiyo imetokea kiasi cha kilomita 30 kutoka mji wa Charlottesville, Virginia.

Wabunge hao walikuwa wanaelekea kwenye jumba la mapumziko katika jimbo la Virginia Magharibi kujadili sheria mpya ya kodi na jinsi ya kuboresha miundo mbinu ya taifa.

Rais Donald Trump anatarajiwa kuungana na wabunge hao katika mkutano huo Alhamisi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG